Nov 01, 2021 03:07 UTC
  • Wanachuo wa Iran waunga mkono kauli ya waziri wa Lebanon dhidi ya Saudia

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametangaza kuunga mkono matamshi ya Waziri wa Habari wa Lebanon, George Kordahi ya kulaani mashambulio ya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen.

Wanachuo hao walikusanyika nje ya ubalozi wa Lebanon hapa mjini Tehran, ambapo wamesisitiza kuwa wanaunga mkono kauli ya waziri huyo wa Lebanon aliliyoyatoa katika mahojiano na kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar.

Wanafunzi hao wa baadhi ya Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu huku wakiwa wamebeba bendera za Lebanon,Iran, harakati ya Hizbullah na Yemen aidha wamesikika wakipiga nara za kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Yemen.

Kadhalika walikuwa wamebeba mabango yenye jumbe za kulaani tawala za Saudia, Israel na Marekani, na kuwapa matumaini wananchi wa Yemen wakisisitiza kuwa, kama Uislamu nao wataibuka washindi. 

Wanachuo wa Iran nje ya ubalozi wa Lebanon mjini Tehran

Waziri wa Habari wa Lebanon, George Kordahi wiki iliyopita, sambamba na kulaani mashambulio hayo ya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, alisisitiza kuwa, kufanya juhudi za kuhuisha uhusiano wa kihistoria kati ya Lebanon na ndugu zake wa Kiarabu ni kipaumbele cha siku zote cha serikali ya Beirut.

Tayari kadhaa wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kama vile Imarati, Bahrain na Kuwait, zimechukua hatua ya kuwaita nyumbani mabalozi wao walioko Beirut kufuatia mzozo huo, zikifuata mkumbo wa Saudi Arabia.

Tags