Nov 01, 2021 03:09 UTC
  • Aal-Khalifa yashadidisha ukandamizaji dhidi ya Wabahrain

Vikosi vya usalama vya utawala wa Aal-Khalifa nchini Bahrain vimewatiwa mbaroni wanaharakati wengine wa kisiasa wanaoupinga na kuukosoa utawala huo wa kiukoo.

Chama kikuu cha upinzani cha al-Wefaq ambalo ndilo kundi kubwa zaidi la Kiislamu nchini humo kimetangaza kuwa, maafisa usalama wa Aal-Khalifa jana Jumapili 'walimuita' Sayyid Ibrahim Kamaluddin, mkuu wa zamani wa Kamati ya Kitaifa ya Umoja, kwa kupinga kufanywa wa kawaida uhusiano wa Manama na Tel Aviv.

Taarifa ya al-Wefaq imeeleza kuwa, shakhsia wengine wawili wa upinzani Abdul Majid Abdul Mohsen, na Ali Mahna waliitwa na maafisa usalama wa Manama hiyo jana, eti kwa ajili ya kusailiwa.

Inaarifiwa kuwa, wawili hao walikamatwa kwa kushiriki matembezi ya amani ya kwenda kumzika Ali Qambar, mfungwa wa kisiasa aliyeaga dunia Jumatatu iliyopita kutokana na maradhi ya saratani. Qambar aliripotiwa kuteswa na kunyimwa matibabu alipokuwa kizuizini.

Wabahrain wakipinga uhusiano wa kawaida na Wazayuni

Kadhalika askari wa Bahrain waliwatia nguvuni raia wengine wawili jana Jumapili katika muendelezo wa kamata kamata zao, ingawaje mashitaka yanayowakabili hayajawekwa wazi hadi sasa.

Wananchi wa Bahrain ambao wamekuwa wakiandamana dhidi ya serikali ya Manama tokea Februari 2011 wanaitaja hatua ya utawala wa kifamilia wa Aal-Khalifa ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala khabithi wa Israel kuwa ni doa jeusi kwa taifa lao.

Tags