Nov 10, 2021 06:15 UTC
  • Abdul Latif al-Qanoua
    Abdul Latif al-Qanoua

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislmu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, hali mbaya ya mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika korokoro za Israel utazucha cheche za mlipuko wa vita na utawala huo ghasibu.

Abdul Latif al-Qanoua amesema harakati za mapambano za Palestina zinafuatilia kwa karibu hali ya mateka wa Kipalestina katika korokoro za Israel hususan wale wanaofanya mgomo wa kula na kwamba zitakuwa mstari wa mbele kutetea matakwa yao. 

Al-Qanoua amesema kuwa, hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kupuuza mashaka yanayowapata Wapalestina hao ambayo yanaongezeka kila siku kutokana na mgomo wa chakula, ni kielelezo cha sura chafu ya utawala wa Israel. mateka wa Kipalestina

Maelfu ya Wapalestina wanaendelea kuteseka katika magereza za Israel

Msemaji wa Hamas ameongeza kuwa, wanamapambano wa Palestina wana turufu zinazoweza kubadili mlingano wa nguvu na kuudhalilisha utawala wa Kizayuni.

Makundi ya mapambano ya Palestina yametangaza kuwa, kamwe hayatawaacha peke yao mateka wa Kipalestina wanaoteseka katika magereza za Israel na kwamba jitihada zinafanyika za kuhakikisha wanaachiwa huru. 

Utawala haramu wa Israel umezidisha mbinyo na ukandamizaji dhidi ya mateka wanaoshikiliwa katika jela na magereza zake baada ya mateka sita wa Kipalestina kutoroka gereza lenye ulinzi mkali la Gilboa tarehe 6 Septemba mwaka huu na kutoa pigo kali kwa mfumo wa usalama wa Israel.

Tags