Nov 11, 2021 08:03 UTC
  • Hizbullah yaitaka Saudia iache kuingilia mambo ya ndani ya Lebanon

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameitaka Saudi Arabia ikome kabisa kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo, huku mgogoro wa kidiplomasia baina ya nchi mbili hizo za Kiarabu ukiendelea kutokota.

Sheikh Naeem Qassim alisema hayo jana Jumatano katika mahafali ya kuwatunukia wanafunzi waliofuzu vyeti na zawadi na kuongeza kuwa, "Lebanon ni nchi huru, ambayo haikubali kuburuzwa na yeyote."

Shaikh Qassim ameeleza kuwa, Saudia ndiyo iliyoanzisha mzozo uliopo baina ya nchi mbili hizo na kubainisha kuwa, Beirut haina ombi lolote kwa Riyadh isipokuwa kuitaka iache kuingilia mambo ya ndani ya Lebanon. 

Amesisitiza kuwa, Saudi Arabia inapaswa kuliomba radhi taifa la Lebanon kutokana na mienendo yake ya kiuhasama dhidi ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.

yaliyotolewa na Waziri wa Habari wa Lebanon, George Kurdahi

Jumapili iliyopita, kiongozi huyo wa kidini nchini Lebanon alieleza kuwa, hatua za kiuhasama zilizochukuliwa hivi karibuni na Saudia dhidi ya Lebanon zimetokana na hamaki za Aal-Saud kushindwa kudhibiti maamuzi muhimu ya kisiasa ya Lebanon, licha ya kumwaga fedha nyingi kwa waungaji mkono wake.

Alisisitiza kuwa, mlengwa mkuu wa hujuma ya kidiplomasia ya Saudia dhidi ya Lebanon ni harakati ya muqawama ya Hizbullah. Hivi karibuni, Riyadh ilitangaza kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na Beirut, kufuatia matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Habari wa Lebanon, George Kurdahi kuhusu vita vya muungano wa Saudia dhidi ya Yemen. 

Tags