Nov 12, 2021 02:22 UTC
  • Ismail Hania: Tunapambana kufa na kupona kuhakikisha mateka wa Kipalestina wanaachiliwa huru

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, suala ka kuachiliwa huru mateka wa Kipalestina ni miongoni mwa mambo yanayopewa kipaumbele na harakati hiyo.

Ismail Hania ameeleza kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS  inafuatilia kwa karibu matukio yanayohusiana na matreka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala haramu wa Israel hususan matreka wanaofanya mgomo wa kula chakula na kwamba, inachukua hatua za lazima za kuachiliwa huru mateka hao.

Kiongozi huyo wa Hamas amesema kuwa, katika sikuu za hivi karibuni harakati hiyo imekuwa katika mawasiiliano na baadhi ya mataifa kuhakikisha kuwa, mateka wa Kipalestina wakiwemo wale wanaoshikiliwa pia nchini SDaudi Arabia wanaachiliwa huru.

Ismail Haniai, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

 

Hivi karibuni Ismail Hania alisema pia kuwa, Hamas haitaruhusu kuwepo masuala ya kimirengo na ya kuwagawa kimakundi mateka wanaoshikiliwa katika jela za Israel, na kwa mara nyingine tena akaitanabahisha jamii ya kimataifa juu ya wajibu ilionao wa kulinda maisha na usalama wa mateka Wapalestina walioko kwenye magereza ya utawala haramu wa Israel.

Shirika la magereza ya utawala haramu wa Kizayuni, na hasa baada ya kukimbia mateka sita Wapalestina katika jela moja ya utawala huo dhalimu, limeshadidisha hatua za uvunjaji sheria linazochukua dhidi ya mateka Wapalestina na kutoa adhabu kali za mateso dhidi ya mateka hao.

Takwimu za jumuiya inayoshughulikia masuala ya mateka wa Palestina zinaonyesha kuwa, hivi sasa kuna Wapalestina wapatao 4,850, wakiwemo watoto 225 na wanawake 41 wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel.

Tags