Nov 12, 2021 07:52 UTC
  • Sayyid Hassan Nasrullah
    Sayyid Hassan Nasrullah

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa nchi za Kiarabu hatimaye zimekiri kwamba Syria imeibuka na ushindi.

Katika hotuba yake ya jana iliyotolewa kwa mnasaba wa Siku ya Shahidi, Sayyid Hassan Nasrullah ameitaja siku hiyo kuwa ni dharuba kubwa ya wanamapambano wa Lebanon kwa adui Mzayuni. Amasema mashahidi walikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Muqawama dhidi ya njama ya kigaidi ya Marekani eneo la Magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa: Katika siku za karibuni kumeripotiwa habari za mamasiliano ya baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu na Rais Bashar Assad wa Syria, suala ambalo ni sawa na kukubali na kukiri ushindi wa serikali ya Damascus, na vilevile kukiri kwamba mradi wa nchi za Kiarabu uliogharimu mabilioni ya dola, umefeli. 

Katika upande mwingine Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, mazoezi kijeshi yanayofanywa mara kwa mara ya na Israel huko kaskazini mwa Palestina inayokkaliwa kwa mabavu ni kielelezo cha wasiwasi na woga wa utawala huo mkabala wa Lebanon  na kuongeza kuwa, mazoezi hayo ya kijeshi yanaonesha kuwa Israel ina hofu kwamba Lebanon inaweza kushambulia makoloni ya ya utawala huo huko al Jalil na kwa sababu hilo kila mwezi inafanya mazoezi ya kijeshi katika eneo hilo.

Sayyid Nasrullah amesema, utawala haramu wa Israel unataka kutimiza njama zake kupitia njia ya kuanzisha uhusiano na nchi za Kiarabu. Amesisitiza kuwa nchi zinazoanzisha uhusiano na utawala huo ghasibu haziwezi kulinda usalama wa Israel.    

Tags