Nov 26, 2021 10:35 UTC
  • Kurejea Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu; kushindwa siasa za kuvuruga usalama wa eneo

Mwanachama wa Kamisheni ya Usalama wa Kitaifa na Siasa za kigeni ya Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema ombi la nchi za Kiarabu la kutaka Syria irejeshwe katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League, ni alama ya kushindwa siasa za kuvuruga usalama na kutaka kubadilisha muundo wa siasa nchini Syria.

Abulfazl Amui, mwanachama wa Kamisheni ya Usalama wa Kitaifa na Siasa za kigeni ya Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameashiria miito inayotolewa na nchi za Kiarabu za kutaka kurudishwa Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kusema: Syria ni nchi iliyo na historia ndefu na kongwe katika ulimwengu wa Kiarabu na bila shaka kusimamishwa uanachama wa nchi hiyo katika jumuiya hiyo kulitokana na matashi ya kisiasa.

Bwana Abulfazl Amui ameongeza kuwa katika mazingira ya sasa mbapo Syria imepata ushindi mkubwa dhidi ya magaidi wanaodhaminiwa na kuungwa mkono kwa hali na mali na nchi za Magharibi na utawala ghasibu wa Israe, na hivyo kuimarika kisiasa ndani ya nchi na katika ngazi za kimataifa, inapasa kurudishiwa nafasi yake halisi katika jumuiya zote za kieneo na kimataifa.

Kikao cha Arab League

Amui amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa muungaji mkono mkuu wa taifa na serikali halali ya Syria na kwamba juhudi zinazofanywa na maadui kwa ajili ya kuifuta nchi hiyo katika ramani ya siasa ni suala lisilowezekana na linalokwenda kinyume na sheria za kimataifa.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Arab League walichukua uamuzi wa kusimamisha kwa muda uanachama wa Syria katika kikao chao kilichofanyika mjini Cairo Misri Novemba 12 2011.

Tags