Nov 27, 2021 12:32 UTC
  • Nasrullah: Ushindi wa mwaka 2000 uliiletea Lebanon uhuru wa kujitawala

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria kukombolewa katika mwaka 2000 maeneo ya ardhi ya nchi hiyo yaliyokuwa yakikaliwa kwa mabavu na akasema: "ushindi huo umeiletea nchi yetu uhuru wa kujitawala na kuipa uthabiti haki yake ya mamlaka ya utawala."

Sayyid Hassan Nasrullah amesema katika hotuba "tungali tuko kwenye kitovu cha mapambano kwa ajili ya kujitawala, kuwa na uhuru na mamlaka yetu na tutaendeleza mapambano haya"; na akaongezea kwa msisitizo: "madamu Lebanon iko kwenye mduara wa vitisho vya Israel, sisi tutaendeleza mapambano bila kujadiliana na yeyote ili kuhakikisha nchi yetu inajitawala na kuwa huru."

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake hiyo, Katibu Mkuu wa Hizbullah  amesema, kuwekwa jina la harakati hiyo kwenye orodha ya makundi ya kigaidi kunaweza kuwa na uhusiano na matukio ya eneo au uchaguzi wa bunge wa Lebanon na akafafanua kwamba "kujiingiza waziwazi Israel kaskazini mwa Afrika kutasababisha hatari kadhaa kwa nchi za Kiarabu za eneo hilo ikiwemo Algeria; lakini kwa upande wa vikwazo na kuliweka jina la Hizbullah kwenye orodha ya makundi ya kigaidi hakutaathiri hata chembe azma na irada ya muqawama."

Sayyid Hassan Nasrullah amezungumzia pia hujuma zilizoratibiwa zinazofanywa dhidi ya Hizbullah na akasema, katika katika miezi na wiki za karibuni, zimefanyika hujuma kubwa za kuishambulia Hizbullah na hilo si jambo geni, lakini lililo jipya ni ukubwa wa hujuma hizo likiwemo suala la kile kinachoitwa "nyaraka".

Kuhusiana na suala hilo, Nasrullah ameashiria nyaraka zilizotolewa katika wiki za karibuni dhidi ya Hizbullah, ambazo amesema ni za kughushi na akabainisha kwamba: walioghushi nyaraka hizo ni wataalamu katika fani hiyo na si Walebanoni; na nyaraka hizo zina maelezo machafu sana ndani yake.

Ameongeza kuwa, kinachosikitisha zaidi ni baadhi ya watu wajinga na majahili kuzitumia nyaraka hizo kama hoja na ushahidi.../

Tags