Dec 03, 2021 04:24 UTC

Mkuu wa Utamaduni wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq maarufu kama Hashd al Sha'abi amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio nguzo ya ulimwengu wa Kiislamu na mrengo wa muqawama na mapambano ya Kiislamu.

Sayyid Hashem al-Heydari alisema hayo jana Alkhamisi katika mji wa Kerman, kusini mashariki mwa Iran na kuongeza kuwa, kuna haja kwa jamii za Waislamu kote duniani kufungamana na kupenda Wilaya.

Amesisitiza kuwa, Iran ndio matumaini ya kambi ya muqawama katika nchi za Iraq, Syria, Lebanon na katika nchi na maeneo mengine ya Kiislamu duniani.

Sayyid al-Heydari ameashiria kipindi alipofanya kazi na Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kubainisha kuwa, "kwa mtazamo wangu, nguzo kuu ya historia na ujio wa Uislamu ni kuwepo mfumo madhubuti wa Wilaya, na Shahidi Hajj Qassem Soleimani alikuwa mtu wa Wilaya na si kiongozi wa Jihadi tu."

Mrengo wa muqawama

Mkuu wa Utamaduni wa Harakati ya Hashd al Sha'abi ya Iran ameongeza kuwa, baadhi ya watu apo katika medani za Jihadi kwa shabaha ya kuyahami mataifa na makabila yao, lakini Haji Soleimani alikuwa shakhsia aliyepigania Wilaya.

Sayyid al-Heydari amesisitiza kuwa: Njia ya Imam Khomeini (MA) haipo tu Iran, lakini nyayo zao zinaendelea kufuata katika mirengo yote ya muqawama na ulimwengu wa Kiislamu, na damu ya Shahidi Soleimani imelipa nguvu jeshi letu.

Tags