Dec 03, 2021 04:26 UTC
  • Licha ya kujitweza, Saudia na UAE zinamdhalilisha Mansour Hadi

Licha ya rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kutoroka nchi, Abdu Rabbuh Mansour Hadi kujipendekeza na kujitweza kwa Saudi Arabia na Imarati, lakini watawala wa Riyadh na Abu Dhabi wameendelea kumdhalilisha na kumtolea vitisho mwanasiasa huyo wa Yemen mwenye umri wa miaka 76.

Abdul Aziz Jabbari, Naibu Spika wa kile kinachoitwa Bunge la Wawakilishi huko kusini mwa Yemen amefichua kuwa, Saudia na Imarati zinamtusi na hata kumdunisha rais Hadi.

Jabbari ameeleza bayana kuwa, licha ya Hadi kujikomba kwa watawala wa Riyadh na Abu Dhabi, lakini madikteta hao wa Kiarabu wamekataa katakata kuiruhusu serikali ya rais huyo mtoro wa Yemen kusafirisha nje gesi asilia au mafuta ghafi.

 

Vita vya Saudia dhidi ya Yemen

Amesema wakuu wa tawala hizo mbili za kidikteta wamekataa kumruhusu Hadi kulihami na kulizatiti kwa silaha jeshi, huku mzozo baina ya pande mbili hizo ukizidi kuwa mkubwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, mtandao wa al Arabi al Jadid ulizinukuu duru za habari zilizofichua kwamba, viongozi wa utawala wa kiimla wa Riyadh, walimteua Abdulmalik al Mekhlafi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Mansour Hadi, lakini rais huyo wa zamani wa Yemen alipinga uteuzi huo.

Tags