Dec 03, 2021 04:27 UTC
  • Jihad al-Islami: Kuanzisha uhusiano na Israel ni kutoa huduma ya bure kwa Wazayuni

Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina imetangaza kuwa, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni kutoa huduma ya bure kwa Wazayuni magharsibu.

Hayo yameelezwa na Dawud Shihab mmoja wa viongozi wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina  ambaye amesisitiza kuwa, hivi sasa katika eneo la Quds Mashariki linalokaliwa kwa mabavu kunafanyika utokomezaji wa kizazi na dhulma dhidi ya wakazi asili wa ardhi hiyo takatifu.

Kongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina sambamba na kuashiria kwamba, hatua zote za utawala vamizi wa Israel ni batili amesema kuwa, njia ya kweli ya kukabiliana na utawala huo ghasibu ni muqawama na mapambano.

Kadhalika Dawud Shihab ameongeza kuwa, kama Wapalestina hawatakuwa na uwezo wa kukabiliana na utawala dhalimu wa Israel basi ulimwengu hauwezi kusikia sauti ya wananchi hao madhulumu.

Maandamano ya kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawakla haramu wa Israel

 

Kiongozi huyo wa Jihad al-Islami amekosoa vikali hatua ya baadhi ya mataifa ya Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa, msimamo huo ni utoaji huduma ya bure kwa adui Israel ambayo imekuwa ikitenda jinai kila uchao huko Palestina.

Aidha akionyesha kusikitishwa na hatua hiyo ya baadhi ya mataifa hayo ya Kiarabu, kongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina amesema kwamba, inahuzunisha kuona kwamba, mataifa hayo sasa yamefika mbali na kutiliana saini hati za makubaliano ya usalama.