Dec 03, 2021 07:49 UTC
  • Ismail Hania: Marekani siyo 'polisi wa dunia', itaendelea kuchezea 'vipigo'

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Marekani siyo 'polisi wa dunia' na kwamba, kuondoka Marekani nhuko Afghanistan kutafuatiwa na kuondola taifa hilo katika maeneo mengine.

Ismail Hania amebainisha kuwa, Marekani na waitifaki wake kinara wao ukiwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamedhoofika mno na wanaendelea kudhoofika siku baada ya siku na hilo ni pigo jingine kwa utawala wenye kupenda makuu ya Washington.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS  amesema hayo katika hotuba yake kwenye Mkutano wa 12 wa Walioko Mstari wa Mbele Quds uliofanyika nchini Uturuki na kusisitiza kuwa, Upanga wa Quds hautawekwa chini mpaka ardhi zote za Palestina, Quds na Msikiti wa al-Aqswa vitakapokombolewa.

Hania ameashiria Vita vya Seif al-Quds vilivyotokea mwezi Mei mwaka huu na kueleza kwamba, vita hivyo lilikuwa tukio muhimu katika njia ya mapambano na adui Mzayuni.

Wanajeshi wa Marekani wakiondoka Afghanistan

 

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameongeza kuwa, kuondoka Marekani huko Afghanistan kutafuatiwa na kuondoka nchi hiyo katika maeneo mengine ya dunia.

Aidha amesisitiza kuwa, Marekani siyo polisi wa dunia na hivi sasa baada ya kupata pigo huko Afghanistan haipaswi kujigamba na kutaka kujionyesha kwamba, ni polisi ya dunia.

Mataifa mbalimbali ya dunia iikiwemo Russia imekuwa ikikosoa hatua ya Marekani kujifanya polisi wa dunia, na kuchukua nafasi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kwamba, hilo jambo lisilokubalika hata kidogo.