Dec 04, 2021 11:23 UTC
  • Ofisi ya Haki za Binadamu Yemen yalaani mauaji ya Saudi Arabia na washirika wake

Ofisi ya Haki za Binadamu katika mkoa wa Taizz nchini Yemen imelaani vikali jinai za utawala vamizi wa Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya wananchi wa Yemen.

Taarifa ya Ofisi ya Haki za Binadamu katika mkoa wa Taizz Yemen imetolewa baada ya ndege za kivita za muungano vamizi wa Saudi Arabia kudondosha mabomu katika wilaya ya Maqbanah mkoani Taiz na kuua raia wasiopungua 30 na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Ofisi ya Haki za Binadamu katika mkoa wa Taizz Yemen imeitaja hujuma na mashambulio ya Saudia na washirika wake pamoja na mauaji yanayofanywa dhidi ya wananchi wa Yemen kuwa ni jinai za kivita.

Jinai ya jana Ijumaa ya Saudia huko Taizz imeendelea kulaaniwa kieneo na kimataifa baada ya watu 30 wakiwemo watoto wadogo kuua kufuatia mashambulio ya anga ya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawaa wa Aal Saud.

 

Kufuatia uungaji mkono wa Marekani, Imarati, utawala haramu wa Israel na nchi nyingine kadhaa za Kiarabu, Saudi Arabia iliivamia kijeshi nchi masikini ya Yemen mnamo Machi 2015 na kuiwekea mzingiro wa pande zote wa nchi kavu, anga na majini. Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia nchi masikini ya Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa.

Hadi hivi sasa uvamizi huo wa Saudia na waitifaki wake umeshasababisha makumi ya maelfu ya Wayemen kuuawa, wengine wengi kujeruhiwa huku mamilioni ya wengine wakiwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.