Dec 05, 2021 06:19 UTC
  • Kuwait yapiga marufuku meli za Israel kutia nanga nchini humo

Serikali ya Kuwait imezipiga marufuku meli za kibiashara zinazobeba bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel kutia nanga katika bandari za nchi hiyo au kubeba bidhaa kutoka Kuwait kuelekea Israel.

Waziri wa Maslahi ya Umma wa Kuwait alitoa amri hiyo jana ambayo imapiga marufuku meli zinazosafirisha bidhaa za utawala haramu wa Israel kubeba au kushusha bidhaa hizo katika bandari za Kuwait. 

Kuwait haiutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel kama nchi na daima huitaja ardhi hizo kuwa ni Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

Kuwait ambayo iliwahi kushiriki katika vita dhidi ya utawala haramu wa Israel imepiga marufuku pia wakazi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kuingia katika ardhi ya nchi hiyo na inawazuia raia wake kushirikiana kwa njia yoyote na Wazayuni maghasibu.   

Tags