Dec 06, 2021 12:48 UTC
  • George Kordahi: Sikuwa mtu wa kwanza kuviona vita vya Saudia huko Yemen kuwa ni upuuzi

Waziri wa zamani wa Habari wa Lebanon aliyejiuzulu hivi karibuni amezungumza kwa mara yaa kwanza katikka mahojiano tangu ajiuzulu na kueleza kwamba, yeye hakuwa mtu wa kwanza kuviona vita vya Saudi Arabia huko Yemen kuwa ni vya kipuuzi na visivyo na maana.

George Kordahi amesisitiza msimamo wake huo na kueleza kwamba, akthari ya wananchi wa Lebanon na mamilioni ya watu katika mataifa ya Kiarabu walionyesha kuwa pamoja na yeye katika kadhia hiyo.

Kordahi amesema kuwa, siku mbili kabla ya kukabidhi barua yangu ya kujiuzulu nilikutana na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati ambaye alinifahamisha kwamba,  kujiuzuulu kwangu ni sharti ambalo limewekwa na Rais Emmanuel Macron kabla hajaanza jitihada za kupatanisha Saudia na Lebanon.

Waziri wa zamani wa Habari wa Lebanon amesema, muda si mrefu ukweli na uwongo utafahamika na kwamba, kujiuzulu kwake hakuwezi kudhamini kurejea uhusiano baina ya Lebanon na Saudi Arabia.

George Kordahi, Waziri wa zamani wa Habari wa Lebanon aliyejiuzulu hivi karibuni

 

Kabla hajateuliwa waziri, Kordahi aliwahi kuikosoa vikali Saudi Arabia kwa kuanzisha vita dhidi ya Yemen na kusema vita hivyo  haviwezi kuendelea milele. Katika mahojiano ya Mwezi Agosti ambayo yalirushwa hewani Oktoba baada ya kuteuliwa waziri, Kordahi alisema vita dhidi ya Yemen ni uvamizi ambao unatekelezwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Alisema vita hivyo ni vya kipuuzi na vinapaswa kusitishwa huku akisema anapinga vita baina ya mataifa ya Kiarabu. 

Matamshi ya Kordahi yaliikera sana Saudia ambayo ilivunja uhusiano wake na Lebanon na hatua hiyo ikafuatwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Kuwait.

Tags