Dec 06, 2021 13:03 UTC
  • HAMAS: 'Maandamano ya Bendera' ya Wazayuni hayawezi kubadilisha utambulisho wa Palestina

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, maandamano ya Wazayuni wakiwa wamebeba bendera za utawala haramu wa Israel hayawezi kubadilisha utambulisho wa Kiarabu na Kipalestina wa ardhi hizo na wakazi asili wa ardhi hizo.

Hazim Qassim, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema hayo katika radiamali yake kwa maandamano ya hivi karibuni ya Wazyuni wakiwa wamebeba bendera za Isarel katika miji ya Ramlah na El'ad na kubainisha kwamba, hatua hiyo ni ya chuki na kibaguzi dhidi ya wakazi asili wa ardhi hizo.

Msemaji huyo wa HAMAS amebainisha kwamba, hatua hiyo ya Wazayuni itasambaratishwa na kusimama kidete na umoja wa Wapalestina na amewataka wakazi asili wa ardhi zilizoghusubiwa mwaka 1948 kujitokeza na kukabiliana na hatua kama hizo zenye lengo la kuzipachika ardhi hizo utambulisho bandia wa Kizayuni.

Hazim Qassim, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

 

Kwa upande wake Muhammad Hamadah, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS katika mji wa Quds amesisitiza kuwa, maandaamano ya bendera ya Wazayuni lengo lake ni kuikarabati sura ya utawala huo ghasibu iliyoharibika.

Amesema maandamano hayo yanafanyika katika hali ambayo, wanamuqawama wa Palestina wamesambaratisha kabisa ile haiba ya Israel baada ya utawala huo kuumbuka na kuchezea vipigo mara kadhaa katika vita na muqawama wa Palestina. 

Abdallah Swiyam mjumbe wa Baraza la Mji huko Quds inayokaliwa kwa mabavu anasema, maandamano hayo ya Wazayuni yatapelekea kushadidi tena mzozo na mivutano katika mji huo mtakatifu.

Tags