Dec 07, 2021 13:16 UTC
  • Jeshi la Yemen: Tumeishambulia Wizara ya Ulinzi ya Saudia huko Riyadh

Msemaji wa Jeshi la Yemen amebainisha kuhusu "oparesheni ya Disemba Saba" na kueleza kuwa vikosi vya ulinzi vya Yemen vimetekeleza oparesheni ya kijeshi ya kipekee huko Riyadh, Jedddah, Taif, Jizan, Najran na Asir katika ardhi ya Saudi Arabia.

Brigedia Jenerali Yahya Saree amezungumzia oparesheni hiyo kwa jina la "Oparesheni ya Disemba Saba" iliyotekelezwa jana Jumatatu na kueleza kuwa tunakabiliwa na ghasia kubwa; na tutatekeleza oparesheni zaidi za kijeshi katika fremu ya kujilinda kwetu kwa mujibu wa sheria katika kujibu kuendelea mashambulizi ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudia na mzingiro dhidi ya Yemen.  

Meja Jenerali Yahya Saree amesema katika Oparesheni ya Disemba 7 jeshi la Yemen limetumia ndege nane zisizo na rubani aina ya 2K Qasaf na makombora mengi ya balistiki kwa ajili ya kuyalenga maeneo nyeti na muhimu huko Abha, Jizan na Najran.  

Msemaji wa jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen jana Jumatatu yaliandika katika ukurasa wa twitter kwamba: vikosi vya ulinzi vya Yemen vimetekeleza oparesheni kubwa na ya kipekee katika ardhi ya Saudia katika kujibu hujuma na mashambulizi ya muungano vamizi wa Saudia na Marekani. 

Muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudia siku kadhaa zilizopita ulishadidisha mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya Yemen ikiwemo katika mji mkuu wa nchi hiyo San'aa; na hadi sasa makumi ya raia wameuawa.  

Mashambulizi ya Muungano vamizi wa Saudia huko Yemen 

 

Tags