Dec 08, 2021 02:33 UTC
  • Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani: Washington haitaondoka Iraq mwishoni mwa 2021

Aliyekuwa naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani David Schenker amedai kuwa, nchi hiyo haina nia ya kuwaondoa askari wake katika ardhi ya Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2021.

Schenker amesema, askari wa jeshi la nchi hiyo wataendelea kuwepo nchini Iraq baada ya kumalizika mwaka 2021 hasa kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini humo hivi karibuni. 

Kwa mujibu wa mpango uliopitishwa na bunge la Iraq na makubaliano yaliyofikiwa baina ya Baghdad na Washington, Marekani inatakiwa ihitimishe kuwepo kwake kijeshi nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, lakini hadi sasa nchi hiyo imekuwa ikitumia kila mbinu na njia ili ikhalifu kutekeleza makubaliano hayo.

Askari wa jeshi la kigaidi la Marekani wakiranda katika mitaa ya miji ya Iraq

Wananchi wengi wa Iraq pamoja na makundi na mirengo ya kisiasa ya nchi hiyo wanataka askari wa jeshi la kigaidi la Marekani waondoke katika ardhi ya nchi yao, kama ilivyoamuliwa katika mpango uliopitishwa na bunge la Iraq Januari 5, 2020.

Askari wa jeshi vamizi la Marekani wamepiga kambi nchini Iraq tangu mwaka 2003. Kambi kubwa zaidi ya jeshi la Marekani nchini Iraq ni ya Ainul-Asad iliyoko mkoani al-Anbar magharibi mwa nchi, na ubalozi wa nchi hiyo uko kwenye eneo lenye ulinzi mkali la Ukanda wa Kijani katika mji mkuu Baghdad.../ 

Tags