Dec 08, 2021 02:34 UTC
  • Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama: Saudia ni ajenti wa ubalozi wa Marekani Beirut

Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema: nafasi haribifu ya Saudi Arabia nchini Lebanon imekuwa kubwa zaidi kuliko harakati chafu za ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut.

Sheikh Maher Hamoud amekieleza kituo cha habari cha al Maa'lumah kwamba nchi yake inashuhudia uingiliaji wa waziwazi wa Saudia na akasisitiza kuwa uingiliaji wa nchi hiyo katika masuala ya ndani ya Lebanon umekuwa mkubwa zaidi kuliko uingiliaji wa ubalozi wa Marekani katika nchi hiyo.

Sheikh Hamoud ameongeza kuwa, Saudi Arabia sasa imegeuka kuwa jicho na sikio la Marekani nchini Lebanon na hali imefikia kiwango ambacho hatari ya harakati chafu zinazofanywa na ubalozi wa Marekani mjini Beirut imekuwa ndogo zaidi kulinganisha na hujuma za Saudia.

Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amebainisha kuwa, Saudi Arabia ina taathira haribifu kwa uchumi wa Lebanon na wala haiitakii mema nchi hiyo.

Awali kabla ya hapo, Sheikh Maher Hamoud aliwahi kueleza pia kwamba, kutokana na mitazamo ya kuchochea machafuko ndani ya Lebanon aliyonayo Mohammad Bin Salman; mrithi huyo wa ufalme wa Saudi Arabia hana hamu ya kuikurubisha pamoja mitazamo kinzani kwa ajili ya kutatua matatizo ya Lebanon.../

Tags