Dec 21, 2021 08:18 UTC
  • Shirika la haki za binadamu la al Karama laishitaki Saudi Arabia UN

Shirika la kutetea haki za binadamu la al Karama limetuma ripoti kwa Kamati ya Kukabiliana na Mateso ya Umoja wa Mataifa likieleza kiwango cha juu cha mateso na unyanyasaji unaofanyika katika jela za utawala wa Saudi Arabia.

Ripoti hiyo ya al-Karama, kundi la kutetea haki za binadamu linaloipinga serikali ya Saudia, imeeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu ukiukwaji wa haki za kimsingi za wafungwa na kuitaka kamati hiyo kufanya uchunguzi hasa kutokana na kwamba, utawala wa Saudi Arabia ulitia saini makubaliano ya kupiga marufuku utesaji Septemba 23, 1993.

Ripoti hiyo imekuja baada ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Mateso kuandaa orodha ya masuala kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu na kuutaka utawala wa Saudia kuyashughulikia.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Al-Karama, limeashiria hali ya "Saud Mukhtar Al-Hashimi", "Suleiman Al-Rashudi", "Khalid Al-Rashed", "Muhammad Abdullah Al-Atibi", "Mohammad Al-Qahtani" na "Walid Abu Al-Khair" ambao wamefungwa gerezani kwa sababu tu ya kuukosoa utawala wa Saudia na umeitaka Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Mateso kufuatilia kadhia yao. Vilevile imeitaka kamati huo kuomba maelezo kuhusu hukumu kali zilizotolewa na utawala wa Saudia dhidi ya watetezi wa haki za binadamu.

Tags