Jan 10, 2022 12:03 UTC
  • Wanajeshi magaidi wa Marekani waiba makumi ya malori ya mafuta ya Syria

Duru za kiusalama za Syria zimetangaza kuwa, muungano vamizi unaoongozwa na wanajeshi magaidi wa Marekani umeiba malori mengine 79 ya mafuta ya Syria na kuyaingiza nchini Iraq.

Shirika la habari la SANA limeripoti habari hiyo likizinukuu duru za kiusalama za Syria zikitangaza kuwa, siku ya Jumapili, muungano vamizi unaoongozwa na Marekani umeingiza nchini Iraq makumi ya malori ya mafuta uliyoyaiba nchini Syria.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mbali na malori hayo 79, zaidi ya malori mingine 60 ya mafuta ya wananchi wa Syria yameibiwa na wanajeshi magaidi wa Marekani na kuingizwa nchini Iraq katika kipindi cha siku chache zilizopita.

Wanajeshi magaidi wa Marekani wanaiba kwa nguvu mafuta ya Syria

 

Wizi wa mafuta ya Syria unaoendelea kufanywa na wanajeshi magaidi wa Marekani ni wa kiwango cha juu mno kiasi kwamba kila wiki makumi ya malori ya mafuta ya wananchi wa Syria yanaibiwa na wanajeshi hao katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Syria na kupelekwa kwenye kambi za kijeshi za muungano vamizi unaoongozwa na Marekani na baadaye kusafirishwa nje ya Syria kupitia nchini Iraq.

Wanajeshi vamizi wa Marekani wako nchini Syria bila ya idhini ya serikali halali ya nchi hiyo na bila ya hata kibali cha Umoja wa Mataifa na wanaendelea kuiba maliasili ya taifa la Syria mbele ya kimya cha kutisha cha jamii ya kimataifa na uungaji mkono wa vibaraka wa dola hilo la kiistikbari la Magharibi.

Wizi huo mkubwa wa mafuta ya Syria unafanyika huku wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu wakiendelea kuteseka kwa uhaba wa nishati na baadhi ya wakati magari yanakaa kwenye foleni kwa masaa kadhaa kusubiri kujaza mafuta nchini humo.

Tags