Jan 13, 2022 11:41 UTC
  • Balozi wa Saudia mjini Beirut aropokwa tena akiituhumu Hizbullah ya Lebanon

Balozi wa Saudi Arabia mjini Beiurut ameendelreaza bwajaja zake dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon baada ya kudai kwamba, Hizbullah inafanya mambo yanayoonyesha iko juu ya serikali ya Lebanon

Walid al-Bukhari ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akidai kwamba, kuachwa maumivu na matumaini ya taifa la Lebanon ni kufumbia macho uhakika wa wazi mbele ya Walebanon wenyewe na kukana wazi ukweli ambao msababishaji wake ni hali ya Hizbullah ya kujiona kuwa iko juu ya serikali ya nchi hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa balozi huyo wa Saudia nchini Lebanon kutoa matamshi ya uongo na yasiyo na ukweli wowote dhidi ya Hizbullah ya Lebanon.

Hivi karibuni mwanadiplomasia huyo wa Saudia alidai kwamba, harakati za chama cha Hizbullah ni za kigaidi na kwamba, kufanya kwake mambo kijeshi ni tishio kwa usalama wa taifa wa Kiarabu.

 

Katika kuendelea na bwabwaja zake, balozi Bukhari alisema kuwa, harakati za kisiasa, kijeshi, kiusalama na kihabari za Hizbullah zinakwamisha mamlaka ya kujitawala ya Saudia pamoja na mataifa ya Ukanda wa Ghuba ya Uajemi.

Kabla yake, Salman bin Abdul Aziz mfalme wa Saudia naye aliitaja Hizbullah kuwa ni harakati ya kigaidi ambayo kwa kufuata muamala wa kijeshi katika eneo la Asia Magharibi imekuwa ikitishia usalama wa taifa wa Kiarabu.

Viongoz wa Saudia wameendelea kuituhumu Hizbullah na mataifa mengine katika hali ambayo, utawala huo wa kifamilia umeendelea kufanya mauaji ya kutisha dhidi ya wananchi wa Yemen ambao hawana hatia yoyote.

Tags