Jan 15, 2022 07:30 UTC
  • UN yaonyesha undumakuwili kwa kushinikiza meli ya UAE iliyokamatwa na silaha Yemen iachiwe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeendeleza mwenendo wa undumakuwili kwa kutaka meli ya Imarati iliyokamatwa ikiwa imebeba silaha na zana za kijeshi zilizokusudiwa kupelekwa nchini Yemen iachiwe.

Nchi wanachama wa Baraza la Usalama la UN zimetoa taarifa ya kulaani hatua ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ya kuizuia meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Imarati huku ikiwa imebeba shehena ya silaha, na kutaka meli hiyo na mabaharia wake waachiwe huru mara moja. Meli hiyo ilikamatwa tarehe Pili Januari katika pwani ya Yemen.

Meli ya UAE iliyokuwa na shehena ya zana za kijeshi

Aidha, baraza hilo limezitaka pande zote zitatue suala hilo haraka na kutilia mkazo kile lilichodai kuwa ni umuhimu wa kufanyika kwa uhuru safari za vyombo vya majini katika Ghuba ya Aden na Bahari Nyekundu kulingana na sheria za kimataifa.

Pasi na kuashiria kwamba meli hiyo ya Imarati ilikuwa imebeba silaha na zana za kijeshi na iliingia kwenye eneo la maji ya Yemen bila kibali, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limedai kuwa hatua iliyochukuliwa na Yemen ni tishio kwa usalama wa meli katika Ghuba ya Aden na Bahari Nyekundu.

Brigedia Jenerali Yahya Saree

Baraza la Usalama limetoa taarifa yake katika hali ambayo msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree alitangaza hivi karibuni kuwa, kwa mara ya kwanza vikosi vya ulinzi vya Yemen vimetekeleza operesheni ya aina yake na kufanikiwa kuisimamisha na kuizuia meli ya Imarati iliyokuwa na shehena ya silaha na zana za kijeshi katika eneo la maji ya nchi hiyo.

Saree amebainisha kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba magari na zana za kivita zinazotumiwa dhidi ya wananchi wa Yemen.../