Jan 16, 2022 02:44 UTC
  • Hizbullah: Marekani, Saudia wahusika wakuu wa vita vya kiuchumi dhidi ya Lebanon

Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbuullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Marekani na Saudi Arabia zimeanzisha vita vya kiuchumi dhidi ya Lebanon.

Sheikh Ali Da'mush, Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbuullah ya Lebanon amebainishah kwamba, kuna vita vichafu vya kiuchumi na kifedha vilivyoanzishwa na tawala za Marekani na Saudi Arabia dhidi ya Lebanon.

Aidha ameeleza kwamba, katika vita hivyo, suhula na nyenzo zote zimekuwa zikitumika kwa ajili ya kuwashinikiza wananchi wa Lebanon ili wabadilishe machaguo yao ya kisiasa hasa katika kipindi hiki nchi hiyo ikitarajiwa kufanya uchaguzi wa Bunge baadaye mwaka huu.

Hayo yanajiri sambamba na matamshi ya viongozi wa Saudia Arabia ya kuituhumu Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon na kuendesha vita vya kipropaganda dhidi ya harakati hiyo ya muqawama.

Najib Mikati, Waziri Mkuu wa Lebanon

 

Hivi karibuni Walid al-Bukhari balozi wa Saudi Arabia mjini Beiurut ameendelreaza bwajaja zake dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon baada ya kudai kwamba, Hizbullah inafanya mambo yanayoonyesha iko juu ya serikali ya Lebanon.

Kabla yake, Salman bin Abdul Aziz mfalme wa Saudia naye aliitaja Hizbullah kuwa ni harakati ya kigaidi ambayo kwa kufuata muamala wa kijeshi katika eneo la Asia Magharibi imekuwa ikitishia usalama wa taifa wa Kiarabu.

Viongoz wa Saudia wameendelea kuituhumu Hizbullah na mataifa mengine katika hali ambayo, utawala huo wa kifamilia umeendelea kufanya mauaji ya kutisha dhidi ya wananchi wa Yemen ambao hawana hatia yoyote.

Tags