Jan 16, 2022 11:54 UTC
  • Amir-Abdollahian: Mgogoro wa Syria hauwezi kutatuliwa bila kuzingatia wakimbizi, vikwazo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kama suala la wakimbizi na vikwazo dhidi ya Syria halitazingatiwa, haitawezekana kusimamia utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo kwa njia inayofaa."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo leo mjini Tehran alipokutana na Geir Pedersen mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria. Katika mkutano huo wamebadilishana mawazo kuhusu matukio ya hivi karibuni ya Syria.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemshukuru mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa kutokana na jitihada zake za kufanikisha mazungumzo ya kitaifa na ya amani Syria na kusisitiza kuhusu juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kufanikisha jitihada za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuleta amani Syria. 

Amir-Abdollahian amesisitiza juu ya mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu utatuzi wa kisiasa wa mgororo  na kuongeza kuwa tokea mwanzo wa mgogoro wa Syria, Umoja wa Mataifa umekuwa ukifuatilia utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.

Rais Bashar al Assad wa Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema uwepo ulio kinyume cha sheria wa wanajeshi wa Marekani nchini Syria na pia hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel didi ya nchi hiyo ndio chanzo cha matatizo katika utatuzi wa mgogoro uliopo katika nchi hiyo . Amesema kuna udharura kwa jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kushughulikia masuala hayo.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria amesema hivi sasa kuna uthabiti Syria na kuongeza: "Hivi sasa hakuna upande wowote unaozungumza kuhusu kuupindua mfumo unaotawala Syria." Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuhusu mamlaka ya kujitawala kitaifa na uthabiti wa kisiasa Syria.

 

Tags