Jan 18, 2022 07:17 UTC
  • Undumakuwili wa Umoja wa Ulaya: Mapigano Yemen yanaweza kuhitimishwa kwa njia ya kisiasa tu

Umoja wa Ulaya umetoa taarifa katika radiamali yake kwa mashambulizi ya kuadhibu ya jeshi la Yemen huko Abu Dhabi na kusisitiza kuwa mapigano yanayoendelea Yemen yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya kisiasa tu.

Umoja wa Ulaya bila ya kuashiria jinai za muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia na kuuliwa maelfu ya watu wa Yemen umetangaza kuwa, eti mashambulizi dhidi ya miundombinu ya raia hayakubaliki. Umoja wa Ulaya umedai kuwa mashambulizi hayo yatashadidisha hali ya mgogoro huko Yemen na kudhoofisha jitihada zinazoendelea za kuhitimisha vita nchini humo.   

Jana Jumatatu jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi yalitekeleza mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani katika maeneo muhimu ndani ya ardhi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na kusababisha mlipuko karibu na maghala ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Abu Dhabi (ADNOC)) na mlipuko mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.  

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi washambuliwa na jeshi la Yemen 

Shirika la habari la Imarati limetangaza kuwa, watu watatu wamepoteza maisha na wengine sita wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo. Polisi ya Abu Dhabi pia imetangaza kuwa raia mmoja wa Pakistan na Wahindi wawili wameuawa katika mashambulizi hayo. 

Tags