Jan 20, 2022 08:11 UTC
  • HAMAS: Taifa la Palestina ndilo litakalopata ushindi wa mwisho mbele ya Israel

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, taifa la Palestina ndilo litakalopata ushindi wa mwisho mbele ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Hazim Qassim amesema hayo katika radiamali yake kwa hatua za Israel za kuendelea kuharibu na kubomoa nyumba za Wapalestina na kusisitiza kwamba, Wapalestina wataendeleza mapambano yao dhidi ya Wazayuni na wataibuka na ushindi mbele ya maghasibu hao.

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amebainisha kwamba, adui Mzayuni hawezi kulishinda taifa la Palestina kwa kutumia mbinu kama kudumisha uvamizi na kubomoa nyumba za Wapalestina.

Amesisitiza kuwa, tukitupia jicho hatua na duru mbalimbali za vita na utawala wa Kizayuni wa Israel tunaona kuwa, siasa za kivamizi za utawala huo daima zimekuwa zikishindwa na kugonga mwamba.

Hazim Qassim, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS 

 

Hatua hizo za Israel za kubomoa nyumba za Wapalestina zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina.

Wananchi wa Palestina wamekuwa wakilaani vikali mipango ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ya ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina na kusema kuwa, hatua hiyo ni jinai za kivita.

Israel inaendeleza mipango yake hiyo iliyo kinyume cha sheria katika hali ambayo, Desemba 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Tags