Jan 22, 2022 14:08 UTC
  • Corbyn: Uingereza inahusika na jinai za Saudi Arabia nchini Yemen

Jeremy Corbyn, Mbunge maarufu nchini Uingereza ameilaumu serikali ya nchi hiyo na kusema kuwa, London ni mshirika wa jinai zinazofanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wasio na ulinzi wala hatia huko Yemen.

Shirila la habari la Fars limeripoti habari hiyo leo Jumamosi na kumnukuu Jeremy Corbyn akisema katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, kitendo cha muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia cha kushambulia jela huko Saada Yemen ni jinai kubwa inayopaswa kulaaniwa na kwamba Uingereza nayo inahusika kwenye jinai hizo.

Duru na shakshia mbalimbali wanaendelea kulaani jinai mpya za Saudi Arabia huko Yemen. Jana vyombo vya habari vilitangaza kuwa, zaidi ya watu 170 wameuawa na kujeruhiwa vibaya katika shambulio hilo la kikatili. Shirika la Msalaba Mwekundi limesema idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika jinai hiyo ni zaidi ya watu 100.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa naye amelaani mashambulizi ya ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya jela ya wafungwa katika mkoa wa Sa'ada nchini Yemen.

Jeremy Corbyn

 

Taarifa iliyotolewa na Antonio Guterres imesema shambulizi jingine limesajiliwa nchini Yemen  ambalo limeua raia wakiwemo watoto wadogo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka na wa wazi kuhusu mashambulizi hayo na kuwawajibishwa wahusika.

Vilevile ametoa wito wa kukomeshwa mzingiro wa Saudia na washirika wake dhidi ya bandari na viwanja vya ndege vya Yemen na kuanzishwa tena mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo.