Jan 23, 2022 07:57 UTC
  • Askari wa Marekani walijificha Abu Dhabi baada ya shambulio la jeshi la Yemen dhidi ya Imarati

Msemaji wa kamandi kuu ya jeshi la kigaidi la Marekani CENTCOM amekiri kuwa, askari wa jeshi hilo walikimbilia mafichoni kwa kuhofia uwezekano wa jeshi la Yemen kuishambulia tena Imarati, kufuatia shambulio la makombora na ndege zisizo na rubani za jeshi hilo katika mji wa Abu Dhabi.

William Bill Urban ameeleza katika taarifa kwamba, kufuatia shambulio la Yemen dhidi ya Imarati, askari wa Marekani walikuwa katika hali kamili ya tahadhari kwa muda wa karibu dakika 30 katika kituo cha anga cha Adhafrah, mjini Abu Dhabi kuanzia saa tatu na dakika moja usiku kwa saa za eneo hilo.

Urban ameongeza kuwa, marubani wa Marekani walitakiwa wajiweke tayari na vifaa vya kinga ndani ya muda wa dakika tano, hali ambayo iliendelea kwa muda wa saa 24.

Baada ya Yemen kuionya mara kadhaa Imarati kwamba iache kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kuchochea mivutano nchini humo, duru za habari zilitangaza siku ya Jumatatu iliyopita kuwa, vikosi vya Yemen vimeshambulia kwa makombora na droni viwanja vya ndege vya Dubai na Abu Dhabi.

Kufuatia mashambulio hayo ya kuitia adabu Imarati, vyombo vya habari vya Yemen vilitangaza Alkhamisi usiku na Ijumaa alfajiri kuwa ndege za kivita za muungano vamizi wa kijeshi wa Saudi Arabia zimefanya mashambulio makali na ya kinyama katika mji wa bandari wa Hudaydah magharibi mwa Yemen na dhidi ya jela moja ya muda iliyoko katika mkoa wa Sa'ada. Hadi sasa watu 87 wameripotiwa kuuawa na 266 na kujeruhiwa kutokana na mashambulio hayo.../

Tags