Jan 24, 2022 08:04 UTC
  • Jeshi la Yemen limeshambulia maeneo ya ndani zaidi huko Saudia na Imarati

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi yameteleleza mashambulizi ndani zaidi katika ardhi ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati). Vimesema, jeshi la Yemen litatoa taarifa maalumu masaa machache yajayo.

Televisheni ya al Masirah imetangaza mashambulizi hayo ya jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi huko Saudia na Imarati kuwa makubwa. Muda mchache uliopita tovuti ya habari ya Sabereen imeripoti kuwa, milipuko minne imetokea huko Abu Dhabi. 

Mifumo ya ulinzi wa anga katika mji mkuu wa Imarati Abu Dhabi iliwashwa baada ya makombora mawili ya balistiki kuulenga mji mkuu huo mapema leo asubuhi.

Kombora la balistiki la jeshi la Yemen likielekezwa huko Abu Dhabi 

Wakati huohuo Wizara ya Ulinzi ya Umoja wa Falme za Kiarabu imedai kuwa makombora hayo mawili ya jeshi la Yemen yamesambaratishwa. Hadi sasa hakuna taarifa zozote kuhusu maafa na hasara zilizobabishwa kufuatia mashambulizi ya jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi. Watu walioshuhudia wameeleza kuwa wamesikia kwa uchache milipuko minne ya nguvu huko Abu Dhabi. Huku hayo yakiripotiwa, muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia umetangaza kuwa kombora la balistiki la jeshi la Yemen limepiga mji wa Jizan kusini mwa nchi hiyo na watu wasiopungua wawili wamejeruhiwa. 

Harakakati ya Ansarullah kwa upande wake imesema kuwa imeshambulia maeneo kadhaa huko Saudia kwa kutumia droni na makombora ya balistiki.