Jan 24, 2022 08:17 UTC
  • Sauti ya mlipuko yasikika Baghdad mji mkuu wa Iraq

Duru za habari zimearifu kuwa sauti ya mlipuko imesikika mapema leo magharibi mwa Baghdad mji mkuu wa Iraq.

Sauti ya mlipuko imesikika leo magharibi mwa mji mkuu wa Iraq na karibu na jela ya Abu Ghureib. Hadi tunaingia matangazoni hakuna taarifa yoyote iliyotufikia kuhusu maafa yaliyosababishwa na mlipuko huo. Duru za habari kutoka Iraq aidha zimearifu kuwa mlipuko huo umejiri licha ya kuweko ulinzi mkali wa askari usalama katika maeneo ya kandokando ya jela ya Abu Ghureib. 

Katika upande mwingine, televisheni ya al Nujaba jana iliripoti kuwa askari usalama wa Iraq wamejielekeza kwa wingi katika maeneo ya kandokando ya jela hiyo ili kuzuia mashambulizi ya kigaidi. 

Tags