Jan 28, 2022 03:03 UTC
  • Amnesty International: Jinai ya Saudia kwenye jela ya Saada imefanyika kwa silaha za Marekani

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesisitiza kuwa, mauaji ya jela ya Saada nchini Yemen yalitekelezwa kwa silaha za Marekani kufuatia mashambulizi ya muungano vamizi wa Saudi Arabia.

Ni baada ya Shambulio la Ijumaa iliyopita kwenye jela ya mkoa wa Saada, lililohesabiwa kuwa moja kati ya mashambulizi mabaya zaidi ya muungano wa vita wa Saudia nchini Yemen, kuua watu 91 na kujeruhi wengine 236.

Katika ripoti yake ya jana Alhamisi shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeashiria ukatili huo mbaya uliofanywa na Saudia, Imarati, Marekani na washirika wao huko Saada, Yemen.

Amnesty International imesema katika ripoti hiyo kwamba, muungano vamizi wa Saudia ulitumia risasi za kuongozwa kutoka mbali za Marekani wakati wa shambulio la anga dhidi ya jela ya Saada kaskazini magharibi mwa Yemen.

Kwa mujibu wa Amnesty International, risasi hizo zinaongozwa na miali ya laser na zinatengenezwa na kampuni ya Marekani "Raytheon".

Mauaji ya Saudi Arabia dhidi ya raia wa Yemen

Ripoti hiyo imesema: Muungano vamizi wa Saudia ulifanya mashambulizi makubwa ya anga kaskazini mwa Yemen, ikiwa ni pamoja na katika mji wa Sana'a, katika wiki iliyopita, na kuua makumi ya raia na kuharibu miundombinu na vituo vya huduma za kijamii."

Marekani na utawala haramu wa Israel ni washirika wakuu wa Saudi Arabia na Imarati katika vita dhidi ya taifa la Yemen. 

Tags