Jan 28, 2022 07:18 UTC
  • Mamluki zaidi ya 90 wa Imarati wauawa kusini mwa Yemen

Duru za Yemen zinaarifu kuwa mamluki zaidi ya 90 wa Imarati wameuawa wakati wa kukabiliana na hujuma ya mamluki hao katika mkoa wa Shibwah.

Duru za kijeshi za Yemeni zimetangaza kuwa, mapigano makali yalikuwa yakiendelea hadi jioni ya jana katika mkoa wa Shabwah kati ya mamluki wa Imarati na jeshi la Yemen linaloshirikiana na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah. 

Katika mapigano hayo mamluki zaidi ya 90 wanaofadhiliwa na Imarati ambao wanajiita al A'maliqa wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa.

Ripoti zinasema wapiganaji wa kundi hilo mamluki walikuwa wakifanya jitihada za kupenya na kuingia eneo la magharibi mwa mkoa wa Shabwah ambako walikumbana na kipigo cha jeshi la Yemen na harakati ya Ansarullah.

Saudi Arabia na Imarati zinaendelea kufanya jitihada za kupanua ushawishi wao na kukalia kwa mabavu mikoa ya Al Mahrah na Shabwah huko mashariki mwa Yemen.

Tags