Jan 29, 2022 08:13 UTC
  • Jeshi la Syria lawazuia askari wa jeshi la kigaidi la Marekani kuingia katika mji wa Hasaka

Jeshi la Syria limewazuia askari wa jeshi la kigaidi la Marekani kuingia katika mji wa Hasaka kaskazini mashariki ya nchi hiyo.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limetangaza kuwa, magari mawili ya askari wa jeshi la kigaidi la Marekani yalikuwa yamedhamiria kuingia makao makuu ya mji wa Hasaka, lakini yalizuiwa kufanya hivyo na askari wa vituo vya upekuzi wa jeshi la Syria na kulazimika kuondoka eneo hilo.

Mara kadhaa askari wa jeshi la Syria wameizuia misafara ya wanajeshi wa Marekani kuingia kwenye miji na vijiji vya mkoa wa Hasaka, kaskazini mashariki ya Syria.

Kwa muda mrefu sasa, askari wa Marekani na magaidi wenye mfungamano nao, ambao wamepiga kambi kinyume cha sheria katika eneo la kaskazini na mashariki ya Syria, si tu wanapora maliasili ya mafuta na mazao ya nafaka ya nchi hiyo, lakini pia wanachukua hatua mbalimbali dhidi ya wakazi na askari wa Syria katika eneo hilo.

Askari wa jeshi la kigaidi la Marekani katika ardhi ya Syria

Maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na wanajeshi wa Marekani na wanamgambo wanaoungwa mkono na nchi hiyo waitwao Vikosi vya Kidemokrasia vya Kikurd QASD, yamekuwa kila mara yakishuhudia maandamano ya malalamiko ya raia wa Syria wanaopinga kuwepo wanajeshi hao na washirika wao na hatua za kigaidi wanazochukua.

Serikali ya Syria imeshasisitiza mara kadhaa kuwa wanamgambo hao na wanajeshi wa Marekani hawana lengo jengine wanalofuatilia huko mashariki na kaskazini mashariki ya nchi hiyo isipokuwa kupora mafuta; na wapo katika maeneo hayo kinyume cha sheria.../