Feb 11, 2022 02:31 UTC
  • HAMAS: Tutalipa kisasi cha kuuawa shahidi vijana 3 wa Kipalestina

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema mrengo wa muqawama utalipiza kisasi cha damu za vijana watatu wa Kipalestina waliouawa shahidi hivi karibuni na jeshi katili la utawala haramu wa Israel.

Ismail Haniya sanjari na kutoa mkono wa pole kwa familia za mashahidi hao, amesisitiza kuwa hakuna shaka kwamba mauaji ya vijana hao wa Kipalestina mjini Nablus yatajibiwa.

Haniya ameeleza bayana kuwa, jinai hiyo ya kihaini ni sera iliyofeli na kugonga mwamba, na katu haiwezi kusimamisha nguvu za muqawama wa taifa la Palestina.

Askari katili wa Israel wakimkandamiza ardhini Mpalestina

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya HAMAS ameongeza kuwa, makundi yote ya muqawama yanahisi kuwa yana wajibu na jukumu la kulipiza kisasi cha mauaji hayo ya kikatili.

Vijana hao watatu wa Kipalestina waliuawa shahidi siku chache zilizopita katika operesheni ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Makhfeya mjini Nablus, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibu wa Mto Jordan.

Tags