Feb 14, 2022 03:20 UTC
  • Aboul Gheit: Maambukizi ya corona yamezidisha umaskini katika Ulimwengu wa Kiarabu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amesema janga la corona limezidisha pakubwa umaskini na ukosefu wa ajira miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Ahmed Aboul Gheit alisema jana huko Cairo kuwa, ripoti ya mwaka jana ya Arab League kuhusu nchi za Kiarabu inaonyesha namna kiwango cha uzalishaji kati ya nchi hizo kilivyopungua kwa asilimia 11.5 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka 2019 kutokana na janga la corona.

Janga la corona na athari zake kwa uchumi wa dunia 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ameonegza kuwa, jumuiya hiyo imesema kuwa haijawahi kushuhudiwa kupungua kukubwa kwa aina hiyo kwani hata katika mgogoro wa fedha ulioikumba dunia mwaka 2009 kiwango cha uzalishaji hakikupungua kwa kiasi hicho.  

Katibu Mkuu wa Arab League amesema, matatizo yaliyopo sasa yamezidisha ugumu kwa changamoto zilizokuwa zikizikabili nchi za Kiarabu kabla ya kuathiriwa na janga la corona. Matatizo hayo yamezorotesha zaidi hali ya mambo ya nchi ambazo zinakabiliwa na mapigano na migogoro mikubwa ya kisiasa. 

 

Tags