Feb 24, 2022 03:03 UTC
  • Taliban: Tumeanza kutambuliwa kwa kufunguliwa baadhi ya balozi za kigeni Kabul

Kiongozi mwandamizi wa Taliban amesema, kufunguliwa tena baadhi ya balozi za kigeni katika mji mkuu Kabul ni ishara ya kutambuliwa kundi hilo na jamii ya kimataifa.

Anas Haqqani ameyasema hayo mbele ya hadhara ya wananchi katika jimbo la Khost na kubainisha pia kwamba, hivi sasa wawakilishi wa Taliban wameanza rasmi shughuli zao za kidiplomasia katika baadhi ya nchi zenye balozi za Afghanistan.

Haqqani ameongeza kuwa, mchakato wa kimyakimya wa kuitambua rasmi Taliban unaendelea kutekelezwa na baadhi ya nchi kwa kufunguliwa tena baadhi ya balozi mjini Kabul.

Anas Haqqani

Hata kama hakuna nchi yoyote hadi sasa iliyoitambua rasmi serikali ya muda ya Taliban, huku kila nchi ikisisitiza kuwa kuundwa serikali pana na jumuishi itakayo shirikisha makabila, vyama na makundi yote ya Afghanistan ndilo sharti la kuitambua Taliban, lakini kundi hilo lililotwaa madaraka ya nchi mwezi Agosti 2021 linaitakidi kuwa, kufunguliwa tena baadhi ya balozi za kigeni mjini Kabul na kuanza shughuli za balozi za Afghanistan katika baadhi ya nchi kupitia wawakilishi wake ni sawa na kutambuliwa kusio rasmi kundi hilo na jamii ya kimataifa.../    

Tags