Feb 27, 2022 08:08 UTC
  • Hamas: Zama za ubabe wa Marekani zimefika ukingoni

Mkuu wa sera za kigeni katika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) amesema moja kati ya mafunzo yanayopatikana katika vita vya Russia na Ukraine ni kuwa, zama za ubabe wa Marekani duniani zimefika ukingoni.

Moussa Abu Marzouk mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na ambaye pia ni mkuu wa sera za kigeni katika harakati hiyo ameongeza kuwa, Marekani haiwezi kukabiliana kijeshi na Russia na hivyo imejizuia kuchukua uamuzi wa kuingia vitani.

Korea Kaskazini nayo pia imesema mapigano huko Ukraine yanatokana na tabia yenye kiburi ya Marekani ya kijichukulia maamuzi ya upande mmoja na kuongeza kuwa, Marekani ilikuwa inalenga kuwa na satwa ya juu zaidi ya kijeshi bila kuzingatia wasiwasi wa kiusalama wa Russia.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imesema Marekani huingilia masuala ya ndani ya nchi zingine huku ikilaani nchi ambazo zinachukua hatua za kujihami. Taarifa hiyo ya Korea Kaskazini imesema sera hizo za Marekani ni kielelezo cha kiburi na undumakuwili.

Oparesheni ya kijeshi nchini Ukraine

Kwingineko, Russia imemuita balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Moscow ikimtaka ajieleze kutokana na msimamo wa utawala huo dhidi ya oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia  Mikhail Bogdanov amemuita Alexander Ben Zvi baada ya waziri wa mambo ya nje wa utawala haramu wa Israel Yair Lapid kulaani oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine. Boddanov amesema oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine zinalenga kulinda maeneo yaliyojitangazia uhuru na pia kuhitimisha muundo wa kijeshi wa nchi hiyo.

 

 

Tags