Mar 26, 2022 02:23 UTC
  • Wazayuni walaumiwa kwa kupungua idadi ya Wakristo mjini Quds

Viongozi wa Kikristo wameeleza hofu yao kutokana na kupungua kwa kiwango cha kushtua idadi ya Wakristo katika mji wa Quds (Jerusalem) huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Wadih Abu Nassar, msemaji wa Baraza la Wakuu wa Kanisa Katoliki mjini Quds ameliambia shirika la habari la Anadolu kuwa, Wakristo walikuwa wanaunda asilimia 25 ya wakazi wote wa Jerusalem mwaka 1922, lakini idadi hiyo imepungua hadi chini ya asilimia 1 kwa sasa.

Abu Nassar amefafanua kuwa, idadi ya Wakristo katika mji wa Quds haizidi 10,000, mji wa Wapalestina unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel, wenye wakazi wapatao milioni moja.

Msemaji wa Baraza la Wakuu wa Kanisa Katoliki mjini Quds amefichua kuwa, idadi ya Wakristo mjini hapo imepungua kwa kiasi hicho kikubwa kutokana na mashambulizi ya Mayahudi wenye misimamo ya kufurutu ada dhidi ya Wapalestina.

Waislamu wakifanya ibada ya Swala mjini Quds

Amesema ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni mjini Quds pia ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kupungua idadi ya Wakristo mjini Quds.

Abu Nassar amezikosoa mamlaka za utawala haramu wa Israel kwa kutowawajibisha na kuwabebesha dhima Mayahudi wenye misimamo mikali ya kuchupa mipaka. 

 

 

Tags