Apr 05, 2022 07:17 UTC
  • Ripoti: Israel imewateka nyara watoto 9,000 wa Kipalestina tokea 2015

Utawala wa Kizayuni wa Israel umewateka nyara maelfu ya watoto wa Kipalestina katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Jumuiya ya Wafungwa wa Palestina(PPS) inayosema kuwa, watoto 9,000 wa Kipalestina wametiwa mbaroni na jeshi katili la utawala haramu wa Israel tokea mwaka 2015 hadi sasa.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana Jumatatu imeongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umewakamata watoto 19,000 tangu ilipoanza Intifadha ya Pili, Septemba mwaka 2000.

Taasisi hiyo imesema watoto 160 wa Kipalestina hivi sasa wanashikiliwa katika jela za kutisha za utawala ghasibu wa Israel, huku wakikabiliwa na mateso na udhalilishaji.

Mtoto wa Kipalestina akishikiliwa na wanajeshi katili wa Israel

Kuanzia Septemba mwaka 2000 wakati ilipoanza harakati ya Intifadha ya Pili, watoto zaidi ya 2,300 wa Kipalestina wameuawa shahidi katika mashambulizi ya askari wa utawala haramu wa Israel. 

Utawala haramu wa Israel unaongoza kati ya tawala zinazokiuka sheria za kimataifa kwa kuwakamata watoto, kuwahukumu na kuwapa mateso ya aina kwa aina katika jela za kutisha za utawala huo.

Tags