Apr 26, 2022 03:10 UTC
  • Sana'a: Umoja wa Mataifa ni mshirika wa mzingiro dhidi ya Yemen

Maafisa wa Yemen wameuonyeshea tena kidole cha lawama Umoja wa Mataifa na kuitaja asasi hiyo ya kimataifa kuwa mshirika wa mzingiro dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu.

Hii si mara ya kwanza kwa Umoja wa Mataifa kulaumiwa na hata kutajwa kuwa mshirika wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen. Hilo linatokana na vitendo vya kindumakuwili vya maafisa wa Umoja wa Mataifa vinavyoonyesha wazi kuegemea upande wa muungano vamizi ambao umekuwa ukifanya mauaji kila uuchao huko nchini Yemen.

Abdul Malik al-Ajari, mjumbe wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen amekosoa vikali utendaji dhaifu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kadhia ya Yemen hasa katika suala la usitishaji vita.

Mashambulio ya anga ya Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen

 

Wakati huo huo, Muhammad Abdul Salam, msemaji wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa, jeshi la Yemen na kamati za wananchi zitatoa jibu kali kwa ukiuka wa makubaliano ya kusitisha vita, akigusia vitendo viovu vya muungano wa vita unaoongozwa na Saudia huko Ma'rib.

Usitishaji vita nchini Yemen ulianza kutekelezwa tarehe pili mwezi huu wa Aprili kwa pendekezo la Umoja wa Mataifa lakini muda wote huu muungano vamizi haujaheshimu usitishaji vita huo. Muungano vamizi unaoongozwa na Saudia unaendelea kuuzingira Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sana'a na vile vile hadi sasa umeshazuia meli kadhaa za mafuta za Yemen.

Tags