May 02, 2022 10:41 UTC
  • Syria: Habari ya jaribio la mauaji dhidi ya Rais Bashar al-Assad siyo ya kweli

Vyombo vya habari vya Syria vimetangaza kuwa, habari ya jaribio la mauaji dhidi ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo haina ukweli wowote.

taarifa ya vyombo vya habari vya Syria imetolewa baada ya baadhi ya duru za habari kuripoti asubuhi ya leo kwamba, Rais Bashar al-Assad amenusurika kkifo baada ya kufeli jaribio la mauaji dhidi yake.

Vyombo hivyo vya habari vilieleza kwamba, Rais Assad alinusurika kifo katika jaribio la mauaji wakati alipokuwa akitaka kuelekea katika Msikiti Mkuu wa al-Hassan kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Swala ya Eidul Fitr.

Hata hivyo mtandao wa gazetii la al-Watan la Syria limeripoti leo kuwa, habari ya jaribio la kutaka kuuawa Rais Bashar al-Assad ni uzushi mtupu.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, shirika rasmi la habari la Syria SANA halijaripoti chochote kuhusiana na habari ya jaribio la kuuawa Rais Bashar al-Assad.

Wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh nchini Syria

 

Habari hiyo ilinasibishwa na Kanali ya Televisheni ya al-Manar ya Lebanon ambayo nayo imetangaza kwamba, haijatangaza habari hiyo.

Syria imekuwa uwanja wa mapigano makali tangu mwaka 2011 kati ya vikosi vya jeshi la serikali ya nchi hiyo na makundi ya kigaidi na kitakfiri.

Ripoti nyingi zikiwemo za vyombo vya habari vya Magharibi, zinaonyesha kuwa nchi za Magharibi zimetoa msaada wa silaha, ujasusi na silaha kwa makundi hayo ili kuiangusha serikali ya Syria.

Serikali ya Bashar Al Assad daima imekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel na katika kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina.

Tags