May 16, 2022 07:44 UTC
  • Israel yampiga marufuku kwa miezi minne Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa  ; asema sitakaa kimya

Utawala wa Kizayuni umempiga marufuku kwa miezi minne Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa Sheikh Ikrima Sabri kutokanyaga katika eneo la msikiti huo kutokana na kile ulichokitaja kuwa hatua za Sheikh Sabri za kuuteteta Msikiti Mtukufu wa al Aqsa kibla cha kwanza cha Waislamu.

Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu wa Palestina huko Baitul Muqadas umekuwa ukilengwa na hujuma na mashambulizi haribifu ya utawala ghasibu wa Israel unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu. 

Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa amejibu haraka kitendo hicho cha uhasama na chuki cha utawala wa Kizayuni dhidi yake.  Sheikh Sabri amesema kuhusiana na hilo kwamba na hapa ninamkukuu: "Nitaendelea kuutetea Msikiti wa al Aqsa na wala sitakaa kimya wala kusalimu amri bali nitaendelea kuutetea msikiti huo hadi mwisho wa maisha yangu', mwisho wa kunukuu.  

Huko nyuma Khatibu huyo wa Msikiti Mtukufu wa al Aqsa huko Palestina alisisitiza kuwa, adui Mzayuni ameshindwa kufanikisha na kutekeleza njama na mipango yake haramu licha ya kuendeleza mashambulizi ya uvamizi wa kila uchao dhidi ya raia wa Kipalestina wakazi wa Quds, katika kuyalinda makundi yenye misimamo mikali ya Wazayuni ambayo yanatekeleza hujuma dhidi ya al Aqsa.  

Hujuma za Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa 

Sheikh Ikrima Sabri aidha ameashiria namna walowezi wa Kizayuni pekee yao wasivyo na uthubutu wa kuuvamia na kuuhujumu Msikiti wa al Aqsa bila ya msaada wa wanajeshi wa Israel na kusisitiza kuwa; tunaapsa kuwa makini na macho dhidi ya njama na hila za maghasibi wa Kizayuni."  

Tags