May 17, 2022 02:32 UTC
  • Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ayataka mataifa ya dunia yaisusie Israel

Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameyataka mataifa yote ya dunia kupasisha miswaada ya kuususia utawala ghasibu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.

Muhammad Shtayyeh, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kukwepa kuhukumiwa Israel katika kipindi cha miaka 74 tangu kuasisiwa kwake ni jambo ambalo linaupa kiburi utawala huo bandia cha kufanya jinai, kuendeleza ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuwafanya kila siku wananchi wa Palestina kuzidi kuwa wakimbizi.

Aidha amesema kuwa, umewadia wakati sasa wa kuweka kando siasa za kindumakuwili na kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina mkabala wa utawala vamizi wa Israel unaoikalia kwa mabavu Quds tukufu.

Huku nyuma shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limewahi kutoa matamko mara kadhaa ya kuunga mkono kampeni ya kuususia utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya Wapalestina.

Muhammad Shtayyeh, Wzairi Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina

 

Mwezi Machi mwaka huu, maelfu ya wahadhiri na watafiti wa vyuo vikuu katika nchi mbalimbali duniani wametangaza kuwaunga mkono wanachama wa Jumuiya ya Mitaala ya Mashariki ya Kati MESA kwa kupendekeza mpango wa kuususia utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Asasi mbalimbali za kutetea haki za binadamu zimekuwa zikisisitiza kuwa, msimo wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina ni zaidi ya kukiuka sheria za kimataifa, kwani mbali na kwamba ujenzi huo ni kinyume cha sheria, vilevile unakiuka na kukanyaga haki za binadamu za raia wa Palestina.

Tags