May 19, 2022 07:11 UTC
  • Sultan Haitham atoa amri ya kifalme ya kuimarishwa ushirikiano wa baharini wa Oman na Iran

Sultan Haitham bin Tariq wa Oman ametoa amri ya kifalme ya kupasisha makubaliano ya ushirikiano wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa uchukuzi na usafiri wa baharini.

Uhusiano wa Iran na Oman ni mzuri muda wote licha ya kuweko mizozo mingi katika eneo la Ghuba ya Uajemi na licha ya kuweko njama za Marekani za kueneza chuki dhidi ya Iran. Uhusiano wa Tehran na Muscat muda wote ni wa kuheshimiana na kuzingatia maslahi ya pamoja.

Viongozi wa Oman wanaamini kwamba, kuwa na uhusiano wa karibu na Iran kunatokana na kuangalia mambo katika uhalisi wa wake. Wanaihesabu Iran kuwa ni jirani yao mwenye nguvu katika eneo hili. Nchi mbili za Iran na Oman hazina mzozo wowote wa mpaka baina yao. Kwa upande wake daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiiunga mkono Oman na uungaji mkono huo ni chanya, wa kudumu na wa kulinda historia kongwe ya Oman.

Nchi mbili za Iran na Oman zina uhusiano mzuri tangu zamani

 

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Oman ONA, Sultan Haitham bin Tariq jana Jumatano alionana na maafisa wa masuala ya kibiashara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  na Oman na akatoa amri ya kifalme ya kupasisha ushirikiano wa Muscat na Tehran katika masuala ya uchukuzi na safari za baharini.

Amri hiyo ya Sultan wa Oman imetolewa katika hali ambayo Alireza Peyman-Pak, Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Biashara ya Iran hivi karibuni aliozungumza na mkuu mtendaji wa Shirika la Meli la Oman kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hasa katika suala la kuanzisha shirika la pamoja la meli pamoja na kutumia vizuri uwezo wa nchi mbili wa usafiri wa baharini.

Tags