May 21, 2022 12:31 UTC
  • Televisheni ya Kizayuni: Israel kuchukua hatua dhidi ya Iran ni vitisho vya maneno tu

Televisheni ya Kizayuni ya Kan 11 imesema, madai yote yanayotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwmba utachukua hatua dhidi ya Iran ni vitisho vya maneno matupu.

Kan 11 imegusia majigambo ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni kuhusu kuanzisha vita dhidi ya Iran na kuripoti kuwa, manuva yote inayofanya Israel ni ya kimaonyesho kwa sababu nchi za Magharibi sasa hivi zimeshughulishwa na Ukraine; na utawala wa Kizayuni umebaki peke yake.

Ripoti ya televisheni hiyo ya Kizayuni imebainisha kuwa, kuhusu utayarifu wa kivita pia Israel haina lolote jipya, kwani tangu mwaka 2007 jeshi lake limeandaa mikakati kadhaa kuhusu Iran na kuifanyia mazoezi katika upeo huu na ule. Hivi karibuni pia imefanyia mazoezi ya kijeshi mikakati hiyohiyo, lakini suala la vita dhidi ya Iran ni la kiwango cha maneno matupu.

Askari wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel

Kan 11 imeongeza kuwa, kwa upande wa kiwango cha utayarifu, utawala wa Kizayuni hauwezi kuvuka kiwango ulichojiandaa kwa uratibu na mashauriano na Marekani. Kwa upande wa mazoezi ya kijeshi Israel imetaka kuwaambia wazayuni au washirika wake kwamba inao uwezo huo, lakini haina nia ya kufanya chochote. Televisheni hiyo ya Kizayuni imeongezea kwa kusema: "katika wiki iliyopita hatujaona nia au ishara yoyote kwa Israel ya kutaka kufanya jambo jengine lolote isipokuwa kueleza tu kwamba sisi tupo msitusahau; ingawa nyinyi mumeshughulishwa na Russia na Ukraine.

Wakati hatua unazochukua utawala haramu wa Kizayuni wa Israel zinahatarisha amani ya eneo lote, mkuu wa majeshi ya utawala huo bandia Aviv Kochavi amekiri kuwa Tel Aviv inakabiliwa na vitisho kuanzia Jenin, Palestina inayokaliwa kwa mabavu hadi Esfahan (katikati mwa Iran).../ 

 

Tags