May 27, 2022 11:09 UTC
  • Russia yakosoa uvunjaji sheria wa Israel na hatua yake ya kupora ardhi za Wapalestina

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amekosoa hatua ya Israel ya kuendelea kukiuka sheria, kupora ardhi za Palestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

Vasily Nebenzya ametoa msimamo huo katika kikkao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kueneleza kwamba, hali ya sasa inayoshuhudiwa katika maeneo matakatifu si ya kukubalika hata kidogo.

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amebainisha kwamba, Israel inaendelea kukiuka wazi sheria za kimataifa, inapora ardhi za Wapalestina sambamba na ujenzi wake wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.

Mwanadiplomasia huyo wa Russia ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za maana ili kukomesha vitendo hivyo vya utawala wa Kizayuni wa Israel ambavyo vinakiuka wazi sheria za kimataifa.

Vasily Nebenzya, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa

 

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

Asasi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na baraza lake la Usalama zimeendelea kukosolewa kutokana na kushindwa kuchukua hatua za maana na za kimsingii kukomesha ukiukaji sheria wa Israel huko Palestina hususan uporaji wa ardhi za Palestina sambamba na ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.