May 27, 2022 11:10 UTC
  • Bunge la Iraq lapasisha sheria ya kupiga marufuku kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel

Bunge la Iraq limepasisha kwa kauli moja sheria ya kupiga marufuku ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa Bunge la Iraq, sheria hiyo sasa kuanzisha uhusiano na Israel kunatambuliwa na katiba ya nchi hiyo kuwa ni uhalifu na inatoa adhabu ya kifo kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuhusika na uhalifu huo.

Mohammed al-Halbousi, Spika wa Bunge la Iraq  jana aliwataka Wabunge waupigie kura muswada wa kutambua kuwa ni uhalifu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel na hatimaye Wabunge wameupasisha muswada huo na kuwa sheriai.

Kipengee muhimu zaidii cha sheria hiyo, ni kupiga marufuku kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kutambua kuwa ni uhalifu kuwa na uhusiano wa aina yoyote  na Israel uwe ni wa wa kisiasa, kiusalama, kiuchumi, kiufundi, kiutamaduni na hata kielimu.

Maandamano ya kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel

 

Mara baada ya kupasishwa sheria hiyo, Wabunge walipaza sauti wakipiga nara dhidi ya utawala haramu wa Israel. Wananchi na shakhsia mbalimbali wa Iraq wamelipongeza Bunge la Iraq kwa hatua hiyo, huku harakati za mapambano huko Palestina na Lebanon nazo zikisifu uamuzi huo ambao ni uungaji mkono wa wazi kwa taifa madhulumu la Palestina linalokandamizwa na Wazayuni maghasibu. 

Mwaka 2020 nchi nne za Imarati, Bahrain, Morocco na Sudan zilianzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu unaoendelea kuikaliwa kwa mabavu Quds Tukufu, hatua ambayo iimeendelea kukosolewa na kulalamikiwa vikali.

Tags