May 29, 2022 03:25 UTC
  • Khatibu wa Msikiti nwa al-Aqswa:

Khatibu wa Masjidul-Aqswa amesema kuwa, uamuzi wa Wazayuni wa kufanya "Maandamano ya Bendera" ni hatua ya kichochezi na amesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua ya kuwazuia Wazayuni hao kuingia katika msikiti matakatifu wa al-Aqswa.

Samahat Sheikh Ekrima Sabri amesema kuwa, utawala haramu wa Israel unataka kutunisha misuli na kuonyesha nguvu na kwamba, Baraza la Bawaziri la Israel licha ya kuwa dhaifu lakini linafanya juhudi za kutekeleza matakwa ya makundi yenye misimamo mikali.

Khatibu wa msikiti wa al-Aqswa ameeleza kuwa, waandamanaji hao wamekuwa wakiimba nyimbo na kutoa nara ambazo zinajeruhi na kuchochea hisia za Waarabu na Wapalestina na ameonya kuhusiana na uchochezi huo.

Polisi ya utawala ghasibu wa Israel imetangaza kuwa, itapeleka maelfu ya askari wake huko Quds Mashariki kwa shabaha ya kudhamini usalama ili kuhakikisha maanmdamano hayo yanafanyika kama ilivyopangwa.

Walowezi wa Kizayuni wakiingia katika msikiti wa al-Aqswa

 

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestiina HAMAS imetoa taarifa na kusisitiza kwamba, "ikiwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hautaacha uvamizi wake dhidi ya msikiti wa Al Aqsa na hautaghairisha maandamano ya bendera, katika hali hiyo tutafikisha ujumbe wetu kwa kombora."

Maandamano ya bendera ya utawala wa Kizayuni hufanyika tarehe 10 Mei kila mwaka kwa mnasaba wa kuanza kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni eneo la kale la mji mtukufu wa Baytul Muqaddas.

Wazayuni wanadai eti mji wa Quds ndio mji mkuu wa utawala huo pandikizi. Lakini wananchi wa Palestina wanasema , Quds ndio mji mkuu wa nchi ya Palestina na kwamba upotoshaji wowote ule hauwezi kufifiliza wala kusahaulisha uhakika huo.

Tags