Jun 03, 2022 10:42 UTC
  • Wazayuni wakivamia tena Kibla cha Kwanza cha Waislamu, jamii ya kimataifa kimya!

Licha ya kwamba taasisi mbalimbali za kimataifa zimetoa tangazo rasmi la kusisitiza kuwa Wazayuni hawahusiki kivyovyote vile na maeneo matakatifu ya Wapalestina ukiwemo Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu, lakini kila leo Wazayuni hao wanauvamia Msikiti huo na jamii ya kimataifa imekaa kimya ikiangalia kwa macho tu.

Mamia ya Wazayuni wenye misimamo mikali wameuvamia tena Msikiti wa al Aqsa huku wakipewa ulinzi kamili na wanajeshi wa utawala katili wa Israel. Kila siku Kibla hicho cha Kwanza cha Waislamu kinavamiwa na walowezi wa Kizayuni.

Walowezi hao wanapewa ulinzi kamili na wanajeshi wa Israel na Mpalestina yoyote hana ruhusa ya kulalamikia kivyovyote vile jinai hizo.

Utawala wa Kizayuni unafanya kila uwezalo ili kufanikisha lengo lake la kulazimisha Mtikiti wa al Aqsa uwe mahala pa kutumiwa na walowezi wa Kizayuni wakati wowote wanaopenda.

Shirika la habari la Shahab la Palestina limeripoti kuwa, leo Ijumaa, mamia ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa al Aqsa na kuendesha "ibada" yao ya Talmud karibu na eneo lijulikanalo kwa jina maarufu la Bab al Asbat.

Wazayuni wakifanya jinai ndani ya Msikiti wa al Aqsa

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, polisi na wanajeshi Wazayuni wamemiminwa kwa wingi kwenye eneo hilo ili kuhakikisha walowezi hao wa Kizayuni wanafanya Talmud yao.

Jumapili wiki hii pia, maelfu ya walowezi wa Kizayuni walikivamia Kibla cha Kwanza cha Waislamu huku wakipewa ulinzi kamili wa kijeshi kutoka kwa utawala pandikizi wa Kizayuni.

Mzee mmoja Mpalestina alipohojiwa na vyombo vya habari alisema, ukandamizaji dhidi ya Wapalestina ni mkubwa kiasi kwamba, watoto wa walowezi wa Kizayuni walimtukana na kumvunjia heshima bila ya kujali umri wake mkubwa lakini aliogopa hata kunyanyua mdomo wake kwa kuhofia asije akasingiziwa ni gaidi na kuanza kupigwa marungu na kufanyiwa ukatili mwingine mkubwa na wanajeshi wa Israel.

Tags